1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI: Mapambano yasababisha vifo nchini Lebanon

20 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0E

Vikosi vya serikali nchini Lebanon vimepambana na wanamgambo katika mji wa bandari Tripoli kaskazini mwa nchi na kwenye kambi ya wakimbizi wa Kipalestina.Kwa mujibu wa maafisa wa usalama,hadi watu 19 wameuawa katika mapigano hayo.Miongoni mwa wale waliouawa ni wanajeshi 11.Jeshi limetumia vifaru katika mapigano hayo yalioanza baada ya polisi mjini Tripoli kuivamia nyumba moja,wakiwasaka wezi wa benki.Kwa mujibu wa serikali ya Lebanon wanamgambo wanaopigana ni wanachama wa kundi la “Fatah al-Islam” linaloungwa mkono na wapelelezi wa Syria,dai ambalo linakanushwa na Damascus.Waziri mkuu wa Lebanon,Fouad Siniora amelituhumu kundi la Fatah al-Islam kuwa linajaribu kusababisha hali ya machafuko nchini humo.