1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Treni yaacha njia na kuuwa watu kadha.

19 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cdk6

Islamabad. Kiasi watu 58 wameuwawa na zaidi ya 120 wamejeruhiwa baada ya treni kuacha njia nchini Pakistan. Treni hiyo ya Karachi Express ambayo ilikuwa imejaa abiria wakienda kusherehekea sikukuu , ilikuwa inasafiri kutoka katika mji wa kusini wa Lahore. Maafisa wa shirika la reli wamesema kuwa ajali hiyo imesababishwa na hitilafu katika njia ya treni na wameondoa uwezekano wa hujuma. Wafanyakazi wa uokozi wanajaribu kuwafikia watu ambao bado wamekwama katika mabogi mawili ambayo yameaharibika sana na maafisa wanasema idadi ya watu waliofariki na waliojeruhiwa inaweza kupanda.