1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO: Viongozi wa China na Japan wafanya mazungumzo

11 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAg

Viongozi wa China na Japan wamefanya mazungumzo katika mji wa Tokyo kufuatia ziara ya waziri mkuu wa China Wen Jiabao nchini Japan.

Ziara hiyo inazingatiwa kuwa muhimu katika kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili zenye uwezo mkubwa katika bara Asia.

Bwana Wen Jiabao anafanya ziara yake ya kwanza nchini Japan baada ya mika saba.

Viongozi hao wametia saini mikataba ya nishati na ya kulinda mazingira, katika mkutano wao pia wameahidi kuzingatia uhusiano wa nchi zao baada ya uhusiano huo kuzorota wakati wa utawala wa waziri mkuu wa zamani wa Japan Junichiro Koizumi.

Waziri mkuu wa China Wen Jiabao amefanya ziara nchini Japan baada ya waziri mkuu wake Shinzo Abe kuzuru China mwaka jana.