1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tokyo. Nchi kadha zaingiza fedha katika mfumo wa benki.

13 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZj

Benki kuu ya Japan imeingiza kiasi cha Euro bilioni 3.5 katika mfumo wa benki ili kuepusha upungufu wa fedha. Hii ni sehemu ya juhudi za dunia kuyasaidia masoko ya fedha.

Benki ya Japan imekwisha ingiza kiasi cha Yen trilioni moja katika mfumo wa fedha siku ya Ijuma, wakati benki kuu za Ulaya na Marekani zilipochukua hatua kama hizo.

Hali ya mkanganyiko katika masoko ya fedha imesababishwa na hasara inayoaminika kuwa imetokana na mikopo ya ununuaji wa nyumba nchini Marekani, ama mikopo mikubwa nyumba yenye mashaka. Wachunguzi wa mambo wanasema kuwa wawekezaji wana wasi wasi kuwa hasara hizo zinaweza kuathiri ukuaji wa uchumi wa dunia pamoja na mapato ya makampuni makubwa. Baadhi ya masoko katika nchi za Asia yameanza biashara wiki hii kwa kupata mafanikio kidogo.