1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO: Japan yarefusha msaada wake Iraq

15 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1n

Bunge la Japan limepitisha mswada wa kurefusha kwa miaka miwili mingine msaada wa vikosi vya anga katika operesheni ya kijeshi inayoongozwa na Marekani nchini Iraq.Uamuzi huo umepitishwa,licha ya upande wa upinzani kutoa mwito wa kuvirejesha nyumbani vikosi hivyo.Kiasi ya wanajeshi 200 wa kikosi cha anga cha Japan hurusha ndege za mizigo na wafanyakazi kutoka kituo cha nchini Kuwait hadi Iraq,kwa ajili ya Marekani na washirika wake.Japan ambayo kuambatana na katiba yake haiwezi kushiriki katika mapigano,mwaka jana iliwarejsha nyumbani wanajeshi 600 waliokuwa wakisaidia kazi za ukarabati kusini mwa Iraq.