1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Titanic yakumbukwa kwa makumbusho Belfast

10 Aprili 2012

Miaka 100 tangu meli maarufu ya Titanic ing'oe nanga kutoka bandari ya Uingereza ya Southhampton ikiwa ndio kwanza ni mpya na kuzama siku nne baadaye kugonga mlima wa barafu na kuzama, sasa yakumbukubwa.

https://p.dw.com/p/14aNH
Makumbusho ya Titanic mjini Belfast.
Makumbusho ya Titanic mjini Belfast.Picha: DW

Mkasa wa meli hii iliyokamilika kuundwa tarehe 31 Mei, 1911 katika kiwanda cha meli ya Belfast, sasa umejengewa makumbusho maalum katika mji huo, inayoitwa "Belfast Titanic."

Kiasi ya watu 15, 000 wamefanya kazi kwenye kiwanda cha meli cha Harland & Wolff ndani ya miaka 100 iliyopita. Sehemu kubwa ya watu hao walifanya kazi katika uundaji wa meli ya kifahari ya abiria ya Titanic siku hizo.

Leo hii mtu anapopita kwenye bandari ya Belfast, hatawacha kidogo kusimama na kufikiria meli ya Titanic, maisha na mauti yake. Hilo ndilo linaloigizwa na sauti katika jengo jipya na makumbusho la "Titanic Belfast", mji unaojifaharishia kujenga meli hiyo kubwa kabisa duniani katika zama zake.

Kwa kuwa mji wa Belfast unataka kujitwalia sehemu kubwa ya fahari ya kisa-asili cha Titanic, ndipo ukajitolea kuanzisha maktaba inayotumia njia za kisasa za mawasiliano kuzungumzia yaliyotokea kabla ya ajali ya Titanic: rikodi ya miaka minne ya ujenzi wa meli hiyo.

Simulizi za kihistoria

Kupitia usimulizi katika makumbusho ya "Titanic Belfast", mgeni anarudishwa karne nzima nyuma, mji huo ukiwa umetanda maua yake: viwanda vya meli, vya tumbaku na tabia ya utani wa watu wake.

Meli ya MS Balmoral ikielekea mahala ilipozama Titanic.
Meli ya MS Balmoral ikielekea mahala ilipozama Titanic.Picha: AP

Mgeni mmoja kutoka Marekani, anasema kwamba makumbusho hii ina mguso wa pekee, kwani inaeleza namna mji wa Belfast ulijengeka kihistoria.

 "Ninajiuliza ikiwa walioijenga Titanic iliwahi hata kuwapitikia kuwa meli waliyopoteza jasho, nguvu na muda wao kuiunda ingelikuja ikazama ikiwa bado mpya na kuangamiza maisha ya watu kadhaa pamoja nayo", anasema mgeni huyo.

Titanic si hadithi ya kuhuzunisha tu

Lakini kubwa zaidi kwa makumbusho hii si kuusikitikia mkasa wa kuzama wa Titanic, bali kuyasherehekea maisha yake. Hata kama maisha hayo yalikuwa mafupi, bado yalikuwa maisha yaliyotayarishwa kwa muda mfupi, kwa matumaini na matarajio ya mafundi na watu wake.

"In Nacht und Eis" filamu ya mwaka 1912 inayofanana na hadithi ya kuzama kwa Titanic.
"In Nacht und Eis" filamu ya mwaka 1912 inayofanana na hadithi ya kuzama kwa Titanic.Picha: public domain

Makumbusho hii inaeleza hadithi kwamba miaka 100 iliyopita, watu wa Belfast sio tu walikuwa wamezama kwenye mapigano na migogoro ya Ireland ya Kaskazini, bali walikuwa wamepiga hatua kubwa za maendeleo kiasi ya kuweza kutengeneza meli kubwa za kifakhari kama Titanic.

Kiasi ya paundi za Uingereza milioni 76 zilitumika kwenye ujenzi wa makumbusho hii, ambayo tangu kufunguliwa kwake mwishoni mwa mwezi Machi 2012, imeshavutia mamia kwa maelfu ya wageni kuitembelea, huku ikisubiri kufunguliwa rasmi kwa kumbukumbu za miaka 100 ya kuzama kwa meli ya RMS Titanic.

Mwandishi: Sebastian Hesse
Tafsiri: Mohammed Khelef
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman