1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TIRANA:Rais Bush ataka uhuru wa haraka kwa jimbo la Kosovo

10 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsw

Rais Gorge Bush wa Marekani ameutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua kuhusu hatma ya uhuru wa jimbo la Kosovo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tirana huko Albania rais Bush alisema hakuna muda wa kutafakari kuhusu hatma ya Kosovo panahitajika hatua zichukuliwe na matokeo yake iwe ni uhuru kwa Jimbo hilo linalodhibitiwa na Serbia.

Aliongeza kusema anawasiwasi kuhusu kutofikiwa matarajio ya watu wa jimbo hilo ambako asilimia 90 ya watu wake ni walbania wanaotaka kujitenga na Serbia.

Aidha ameonya, kwamba kunaweza kukatokea ghasia endapo mwafaka hautafikiwa juu ya suala la uhuru wa Kosovo. Mpango wa Umoja wa mataifa wa kutaka jimbo hilo lipewe uhuru unaungwa mkono na Marekani,na Umoja wa Ulaya

Lakini unapingwa vikali na Urussi pamoja na mshirika wake Serbia.Katika mkutano wa hivi karibuni wa viongozi wa nchi tajiri kiviwanda wa G8 rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy alipendekeza kuwepo muda wa miezi sita wa kutafakari suala hilo la hatma ya Kosovo kabla ya kutekelezwa chochote katika mpango wa Artisari.