1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TIBILIS:Urusi yatuhumiwa kuishambulia kwa mabomu Georgia

7 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbN

Georgea imesema kuwa ndege mbili za kivita za Urusi zimeingia katika anga yake na kuangusha mabomu ambayo hata hivyo hayakulipuka.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Georgia Shota Ustiashwili amesema kuwa uvamizi huo ulitokea jana jioni kwa saa za Georgia wakati ndege hizo zilipoingia na kuangusha mabomu katika kijiji cha Tsitelubani kwenye mkoa wa Gori.

Hata hivyo Urusi imekanusha taarifa hizo.