1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Thomas Bach rais mpya IOC

10 Septemba 2013

Thomas Bach ameongeza ushindi mwingine baada ya ule wa medali ya dhahabu katika mchezo wa fencing katika olimpiki ya mwaka 1971 wakati alipochaguliwa kuwa rais wa tisa wa kamati ya olimpiki ya kimataifa IOC.

https://p.dw.com/p/19fcY
Germany's IOC Vice-President Thomas Bach reacts while talking to an IOC member at the125th IOC Session at the Hilton hotel in Buenos Aires, Argentina, 08 September 2013. Photo: Arne Dedert/dpa +++(c) dpa - Bildfunk+++
Thomas BachPicha: picture-alliance/dpa

Bach mwenye umri wa miaka 59 raia wa Ujerumani na ambaye pia ni mwanasheria amesherehekea ushindi wake wa kishindo dhidi ya wagombea wengine watano katika duru ya pili ya uchaguzi katika uchaguzi uliokuwa wa siri wa kamati hiyo ya IOC katika kikao cha 125 leo Jumanne(10.09.2013).

Bach ambaye ni mtu mwenye hamasa kubwa ya kiutendaji alikuwa mtu ambaye anapigiwa upatu kuchukua nafasi ya Jacques Rogge kwa muda mrefu na sasa amenyakua wadhifa huo wa juu katika spoti duniani miaka 22 baada ya kuchaguliwa kuingia katika kamati hiyo ya IOC.

International Olympic Committee president Jacques Rogge holds up the name of Thomas Bach of Germany after he was elected the ninth president of the IOC during a vote in Buenos Aires, September 10, 2013. REUTERS/Enrique Marcarian (ARGENTINA - Tags: SPORT OLYMPICS)
Thomas Bach akitangazwa rasmi kuwa mshindiPicha: Reuters

Kumbukumbu

"Uff!" amesema , katika matamshi yake ya kwanza kama rais wa IOC. "Hii ni ishara kubwa kabisa ya kuonesha imani kwangu na kuniamini.

"Wacha tuwe pamoja katika kundi hili la muziki wa pamoja, tucheze muziki kwa pamoja kwa ajili ya hali bora ya baadaye," ameahidi Bach.

Bach anakumbuka siku zake za kucheza mchezo wa fencing ambazo pia zilimfanya kunyakua ubingwa wa dunia mwaka 1977 mjini Buenos Aires, na aliwashukuru wale ambao hawakumpigia kura na wale waliompigia kura.

"Pia nitafanyakazi kwa ajili yenu na pamoja na nyie katika miaka ijayo na nataka mniamini pia," amesema. Mlango wangu utakuwa wazi, masikio yangu na moyo wangu kila wakati vitakuwa wazi."

Der deutsche Florett-Fechter Thomas Bach sitzt auf einer Bank am 23.04.1972 in Deutschland. Foto: +++(c) Picture-Alliance / ASA+++
Thomas Bach katika michezo ya olimpiki mwaka 1972Picha: picture-alliance/dpa

Rogge ambaye anaondoka amesema katika ufunguzi wa kikao hicho mjini Buenos Aires kuwa "rais mpya atakuwa na wakati mzuri sana katika maisha yake."

Changamoto

Rogge anafahamu kutokana na miaka 12 ya uongozi wake, pia kuwa kuna changamoto mbele ya Bach, ambaye amechaguliwa hadi mwaka 2021 na kisha anaweza kuomba uongozi kwa kipindi cha pili na cha mwisho , cha miaka minne.

BILDAUSSCHNITT! v.l. Franziska SCHENK (Moderatorin), Kip KEINO ( Olympiasieger Leichtathletik, KEN), Fuerst Albert II. VON MONACO, Nadia COMANECI (Olympiasiegerin Turnen, ROM), Pal SCHMITT (Staatspraesident HUN), Dr. Thomas BACH (DOSB-Praesident), Nadia COMANECI (Olympiasiegerin Turnen, ROM) waehrend der Podiumsdiskussion, halbe Figur, Halbfigur, Querformat, Deutscher Olympischer SportBund feiert 30 Jahre Olympischer Kongress am 28.09.2011 in Baden-Baden / Deutschland
Alama ya OlimpikiPicha: picture-alliance/Sven Simon

Changamoto hizo ni pamoja na michezo ijayo ya majira ya baridi mjini Sochi mwaka 2014, huku kukiwa na wasi wasi wa usalama kuhusiana na vitisho vya kigaidi pamoja na utata kuhusiana na upinzani kuhusu mashoga, pamoja na michezo ya mjini Rio mwaka 2016 ambayo imekumbwa na uchelewesho wa ujunzi.

Mageuzi ya wakati wote ya mipango wa michezo ya olimpiki na olimpiki kwa vijana , kuendeleza utajiri mkubwa wa kamati ya IOC katika nyakati ngumu za kiuchumi, na kuhakikisha maadili ya olimpiki dhidi ya matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu pamoja na kupanga matokeo ni majukumu ambayo yanamsubiri Bach.

Bach alitangaza kuwania wadhifa huo Mei 9 akifanya kampeni iliyopewa jina la "Umoja katika hali anuai," lakini alikuwa akiifanya kazi kupanda juu ili kufikia lengo lake la kuwa kileleni mwa kamati ya kimataifa ya olimpiki kwa miaka kadha.

President of the German Olympic and Sports Confederation Thomas Bach speaks during their presentation at the 123rd IOC session in support of Munich's bid to host the 2018 Winter Games in Durban, South Africa, Wednesday July 6, 2011. The International Olympic Committee will announce the host city for the 2018 Winter Olympics in Durban. The IOC members will choose between three candidates Annecy, France; Munich Germany; and Pyeongchang, South Korea for the 2018 host. (Foto:Themba Hadebe/AP/dapd)
Thomas Bach akihutubia kikao cha OICPicha: dapd

Amekuwa makamu wa rais wa OIC kwa miaka kumi chini ya Rogge, akifanyakazi katika tume 14 na alitumia miaka 15 katika bodi yenye ushawishi mkubwa wa utendaji ambayo inatoa maamuzi, alikuwa mwenyekiti wa tume ya sheria na kamati ya nidhamu katika michezo.

Uzoefu wake huu mkubwa na mtandao umemruhusu kufahamu mambo mbali mbali ya matokeo mazuri katika michezo duniani hali ambayo imemfanya kuwa , "chaguo lisilo kuwa na shaka," kwa mujibu wa mjumbe mmoja wa heshima wa IOC Walter Troeger.

Mwandishi : Sekione Kitojo / dpae

Mhariri: Mohammed Abdul rahman