1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

The Hague. Uholanzi kuchangia katika kikosi cha kulinda amani Darfur.

14 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBiz

Uholanzi imesema kuwa inaangalia uwezekano wa kujiunga na jeshi la pamoja la Afrika na umoja wa mataifa la kulinda amani, linalopangwa kuwekwa katika jimbo la Sudan la Darfur.

Hii inafuatia ombi mwezi uliopita kutoka Umoja wa mataifa kwa ushiriki wa Uholanzi.

Uholanzi tayari imetuma maafisa wawili nchini Sudan ili kutayarisha uwezekano wa kutumwa ujumbe huo.

Wakati huo huo , shirika la habari la reuters limesema kuwa mjumbe maalum wa ngazi ya juu wa Marekani katika jimbo la Darfur ameishutumu serikali ya Sudan kwa kushambulia tena maeneo ya raia, na waasi kwa kuzuwia juhudi za kimataifa za kuumaliza mzozo wa Darfur.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Khartoum kufuatia ziara yake katika jimbo la Darfur , Andrew Natsios amesema kuwa pande zote mbili zinapaswa kulaumiwa katika mzozo huo ambao umesababisha mzozo mkubwa kabisa wa kiutu duniani.