1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

THE HAGUE: kesi ya Charles Taylor itaendelea januari mwaka ujao

21 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXF

Mahakama ya mjini the Hague, inayosikiliza kesi ya uhalifu wa kivita inayomkabili aliekuwa rais wa Liberia Charles Taylor, imeahirisha kesi hiyo hadi mwezi januari mwaka ujao.

Mahakimu wa mahakama hiyo inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa wametoa uamuzi huo kuitikia ombi la mawakili wa Taylor juu ya kupatiwa muda zaidi wa matayarisho ya kujitetea.

Taylor anakabiliwa na mashtaka 11 ikiwa pamoja na juu ya kuwatumia watoto kama askari wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone ambapo watu laki moja na alfu 20 walikufa.