1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

THE HAGUE: Dragan Zelenovic ahukumiwa miaka 15 jela

5 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCb

Mahakama ya kimataifa mjini The Hague imemuhukumu kifungo cha miaka 15 jela askari wa zamani wa Serbia kwa makosa ya ubakaji na ukiukaji wa haki za binadamu katika vita vya Bosnia vya mwaka 1992 hadi mwaka 1995.

Dragan Zelenovic alikiri makosa hayo mapema mwaka huu, amesema kuwa alifanya hivyo ili kuwaepusha wahanga kiwewe cha kutoa ushahidi mahakamani.

Zelenovic alihusika katika kampeni ya kuwatesa na kuwabaka wanawake wa kiislamu katika mji wa Foca wa mashariki mwa Bosnia mwaka 1992.