1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madhara siyo makuwa

Admin.WagnerD17 Septemba 2015

Tetemeko kubwa la ardhi limeikumba Chile na Rais wa nchi hiyo Michelle Bachelet amethibitisha kwamba watu wamekufa. Serikali ya nchi hiyo imeamuru watu wahamishwe kutoka maeneo ya pwani.

https://p.dw.com/p/1GXt3
Rais wa Chile Michelle Bachelet
Rais wa Chile Michelle BacheletPicha: Reuters/R. Garrido

Watu zaidi ya milioni moja walilazimika kuondoka majumbani mwao baada ya tetemeko la ardhi lililofikia kipimo cha Richter cha 8.3 kulikumba eneo la pwani la bahari ya Pasifiki nchini Chile.

Tetemeko hilo lilisababisha mawimbi makubwa katika maeneo ya miji ya pwani. Kwa mujibu wa habari watu watano wamekufa.

Serikali ya Chile imeamuru watu wahamishwe kutoka maeneo ya pwani ili kuepusha maafa kama yale yaliyotokea mnamo mwaka wa 2010 kutokana na idara husika kushindwa kuwatahadharisha watu mapema juu ya kimbunga cha Tsunami. Mamia ya watu walikufa wakati huo.

Tetemeko hilo lililotokea jana liliyatikisa majengo na kusababisha mawimbi ya Tsunami yaliyofika hadi Japan. Watu nchini Chile walikimbilia barabarani wakiwa wamejawa hofu.

Gavana wa jimbo la kati la Choapa, Patricio Trigo alikwenda katika wilaya ya Illapel ambako madhara pia yalikuwa makubwa. Amesema majengo mengi yameteketezwa na mama mmoja amekufa. Jimbo hilo la kati la Choapa limetangazwa kuwa la maafa.

Mtu mwengine aliekuwa na umri wa miaka 86 pia alikufa katika mji mkuu wa Chile, Santiago ,umbali wa kilometa 228 kutoka mahala ambapo tetemeko lilianzia.

Hatari ya kutokea tsunami

Kituo kinachotoa tahadhari kilichopo Hawaii kimesema pana uwezekano wa kutokea mawimbi ya Tsunami katika sehemu za pwani za Chile. Kituo hicho kimetahadharsiha kwamba mawimbi ya Tsunami yanaweza kutokea pia katika pwani za Hawaii na sehemu za California nchini Marekani.Lakini Afrika haukutajwa.

Rais wa Chile Michelle Bachelet amekwenda kwenye sehemu zilizoathiriwa zaidi, na tetemeko. Bibi Bachelet amesema kwa mara nyingine Chile imekumbwa na janga la asili. Hata hivyo Rais huyo ameelezea faraja kwamba tetemeko hilo halikusababisha madhara makubwa .Lakini mishtuko mingine ilitokea baada ya tetemeko hilo na sehemu za kati ambazo ni za kilimo na viwanda zilitikiswa .

Präsidentin Chile Michelle Bachelet
Picha: picture-alliance/dpa/M. Ruiz

Chile inatarajia kuadhimisha siku ya uhuru hapo kesho lakini, vyombo vya habari vimearifu kwamba barabara zimeharibika na usafiri umesimamishwa baina ya mji mkuu Santiago na eneo la kaskazini.

Watu zaidi ya 500 walikufa nchini Chile mnamo mwaka wa 2014 kutokana na tetemeko lililosababisha mawimbi makubwa ya Tsunami.

Mwandishi:Mtullya Abdu/rtre,afp

Mhariri:Gakuba Daniel