1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEL AVIV : Rice ziarani Mashariki ya Kati

15 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Fg

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice ameanza ziara ya siku nne Mashariki ya Kati ambayo inakusudia kuweka msingi wa mkutano wa amani unaodhaminiwa na Marekani uliopangwa kufanyika mwezi wa Novemba.

Kabla ya kuwasili kwake mjini Tel Aviv Rice haikuiwekea matumani makubwa ziara hiyo kwa kusema kwamba hategemei kufanikisha uvumbuzi wowote ule mkubwa.Ameanza ziara yake kwa kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert na waziri wa ulinzi Ehud Barak.Pia amekutana na Waziri Mkuu wa Wapalestina Salaam Fayad.

Taarifa zilizotolewa na pande hizo mbili zimedokeza kwamba bado ingali zinatofautiana sana.

Rice pia anatazamiwa kuitembelea Misri na Jordan.