TEL AVIV: Israil yaidhinisha hatua ya kuondoa vizuizi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. | Habari za Ulimwengu | DW | 26.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEL AVIV: Israil yaidhinisha hatua ya kuondoa vizuizi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Baraza la mawaziri la Israil limeidhinisha kuondolewa vizuizi 27 vya barabarani katika eneo la ukingo wa magharibi wa mto Jordan, na hivyo kutekeleza moja ya ahadi alizotoa waziri mkuu Ehud Olmert kwa Rais Mahmoud Abbas. Hatua hiyo itaruhusu uchukuzi huru wa bidhaa katika eneo hilo lililo na mamia ya vizuizi vya barabarani pamoja na vituo vya ukaguzi. Katika mkutano wa kwanza rasmi kati ya Olmert na Abbas siku ya jumamosi, waziri mkuu huyo aliahidi kumkabidhi Abbas dola milioni mia moja za ushuru ambao serikali ya Israil ilikuwa imekataa kuutoa kwa mamlaka ya Palestina. Fedha hizo zitatolewa kwa masharti kwamba zisipitie mikononi mwa serikali inayoongozwa na chama cha Hamas. Kwa sasa hivi Abbas yumo nchini Jordan. Mfalme Abdallah

wa Jordan pia amemwalika Waziri Mkuu wa Palestina Ismail Haniyah kwa mazungumzo kati yake na Abbas juma hili mjini Amman.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com