1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN:Rais wa Iran asema nchi yake aihitaji bomu la nuklia wala vita

24 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBN6

Rais Mahamoud Ahmednejad wa Iran amesema kuwa nchi yake haihitaji kuwa na silaha za nuklia na kwamba haina mpango wa kuingia vitani na Marekani.

Akizungumza katika mahojino na kituo cha televisheni cha Marekani mjini Teheran kabla ya kueleka New York katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais huyo wa Iran amesema kuwa ni makosa kufikiria kuwa Marekani na Iran zinajiandaa kuingia vitani.

Rais Ahmednejad anatarajiwa kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kesho, katika hotuba inayosubiriwa kwa hamu kubwa.

Matamshi hayo ya rais wa Iran yanakuja siku moja tu baada ya kuonya kuwa yoyote atakayejaribu kuishambulia Iran, atajutia uamuzi wake, ijapokuwa alisema, jeshi la nchi hiyo ni kwa ajili ya kujilinda.

Rais huyo wa Iran leo hii anatarajiwa kutoa mhadhara katika chuo kikuu cha Columbia nchini Marekani.