1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN.Rais wa Iran aishustumu Marekani kwenye barua yake

30 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCoF

Rais Mahmoud Ahmednejad wa Iran amewataka Wamarekani wazidishe miito ya kuondolewa wanajeshi wa Marekani kutoka nchini Irak.

Katika barua yake kupitia ubalozi wa Iran katika umoja wa mataifa rais Ahmednejad amesema kuwepo Marekani katika nchi ya Irak kumechangia kuongezeka matendo ya kigaidi.

Kiongozi wa Iran ameshutumu sera za rais Bush kuhusu Mashariki ya Kati na ameitaka nchi hiyo kuitambua ardhi ya Wapalestina.

Katika barua hiyo rais Ahmednejad ameshutumu juu ya kuwepo jela ya Guantanamo Bay iliyo nchini Cuba na kuitaja jela hiyo kuwa imechafua sifa ya Marekani.

Vile vile barua hiyo imeutaka utawala wa rais George Bush kutilia maanani matokeo ya uchaguzi wa hivi karibuni ambapo chama cha Demokratik kimeongeza udhibiti wake katika Congress.