1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN:Rais Putin atoa pendekezo la kutatua suala la nuklia la Iran

17 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ex

Rais wa Urusi Valdimir Putin ametoa pendekezo la kujaribu kumaliza mvutano ulioko kuhusu suala la nuklia la Iran katika ziara yake nchini humo iliyokamilika jana usiku.Tangazo hilo linatokea huku msuluhishi wa ngazi za juu wa Iran kuhusu suala la nuklia Ali Larijani anatangaza kuwa anapanga kufanya mazungumzo na mratibu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Javier Solana ili kujaribu kutafuta suluhu.Mkutano huo unaratajiwa kufanyika mjini Roma nchini Italia.Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu pendekezo hilo lililotolewa wakati Rais Putin alipofanya mazungumzo na Ayatollah Ali Khamenei.

Ziara hiyo iliimarisha zaidi uhusiano kati ya mataifa hayo mawili aidha Urusi kujitenga na kauli kali za mataifa ya magharibi kuhusu mpango wa Iran wa nuklia unaozua utata.Rais Putin alihudhuria mkutano wa mataifa yanayopakana na Bahari ya Caspian na kufanya mazungumzo na viongozi wa ngazi za juu wa Iran ikiwa ni ziara ya kwanza kufanywa na kiongozi wa Kremlin tangu vita vya dunia vya pili.

Usalama mkali ulidumishwa kufuatia madai ya njama ya kutaka kumuua Rais Putin.Bwana Putin aliyaonya mataifa ya magharibi kutoshambulia Iran kwasababu ya mpango wake wa nuklia na kusisitiza kuwa kiwanda cha kwanza cha nukilia cha Iran kilichojengwa na Urusi kitakamilika kama ilivyopangwa na kuunga mkono haki ya taiafa jilo kutengeza nishati ya nuklia.

Taarifa ya pamoja ya viongozi hao inasisitiza umuhimu wa ushirikiano zaidi kuhusu masuala mbalimbali ulimwenguni.