1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN:Iran inavyo vifaa 3000 vya kurutubisha Uranium

3 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTA

Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran ametangaza kwamba nchi yake kwa sasa inadhibiti zaidi ya mashine 3000 za kurutubisha madini ya Uranium katika kinu chake cha Natanz.

Iran imesema lengo lake kuu katika mpango wake wa nyuklia lilikuwa kuwekeza mashine hizo 3,000.

Hata hivyo shirika la kimataifa linalosimamia nguvu za atomiki katika ripoti yake ya hivi punde lilisema kuwa Iran ina kiwango cha chini ya mashine 2000 katika kinu hicho cha Natanz.

Nchi nyingi za magharibi zinahofia kwamba Iran inataka kutengeneza silaha za kinyuklia madai yanayokanushwa na serikali ya Tehran ambayo inasisitiza kuwa mpango wake ni kwa ajili ya matumizi salama ya kiraia.