1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN:Ali larijani ajiuzulu kuwa mpatanishi wa Iran katika mazungumzo ya Nuklia

20 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7E5

Mpatanishi mkuu wa Iran kwenye mazungumzo juu ya mzozo wa Nuklia wa nchi hiyo na nchi za magharibi Ali Larijani amejiuzulu katika wadhifa huo.

Msemaji wa serikali Gholam Hossein Elham amesema Ali Larijani ambaye ni katibu wa baraza kuu la usalama la Iran amejiuzulu lakini hakuna sababu zilizotolewa kutokana na uamuzi huo ingawa amesema bwana Larijani anataka kujishughulisha na masuala mengine ya kisiasa.

Rais Mahmoud Ahmedinejad amekubali kujiuzulu kwa Larijani na naibu waziri wa mambo ya nje anayehusika na masuala ya Ulaya na Marekani Saeed Jalili ndiye atakayechukua mahala pake.

Kwa muda sasa inadaiwa Larijani amekuwa akitofautiana na rais Ahmedinejd juu ya jinsi ya kuendelea na mazungumzo ya Nuklia na nchi za magharibi.Kwa mujibu wa msemaji wa serikali wa Iran Saeed Jalili atashiriki katika mazungumzo na mkuu wa sera za nje za Umoja wa ulaya Javier Solana yaliyopangiwa kufanyika jumanne mjini Roma Italia.