1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Wachunguzi wa Kinuklia wawasili.

14 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2C

Wachunguzi wawili kutoka katika shirika la kimataifa la nishati ya Atomic IAEA, wamewasili nchini Iran.

Shirika la habari la Iran limeripoti kuwa wachunguzi hao wataangalia vinu vya kurutubisha madini ya Uranium katika eneo la Isfahan katikati ya Iran pamoja na kinu kingine kilichoko jirani cha Natanz.

Iran inaripotiwa kuwa imehifadhi kiasi cha tani 280 za gesi ya Uranium katika kinu cha Isfahan, ambayo itahamishwa katika kinu cha Natanz ili kuwekwa katika mashine ambazo zitarutubisha Uranium hiyo.

Iran inatakiwa na baraza la usalama la umoja wa mataifa kusitisha mpango wake huo wa urutubishaji wa Uranium ifikapo mwishoni mwa mwezi wa May.