1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Umaarufu wa Ahmadinejad waanza kupungua

19 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCiG

Wizara ya mambo ya ndani ya Iran imethibitisha ushindi mkubwa wa rais wa zamani wa nchi hiyo Hashemi Rafsanjani katika uchaguzi wa baraza la wataalamu. Kwa mujibu wa matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa Ijumaa iliyopita, Rafsanjani alipata kura nyingi zaidi akilinganishwa na mgombea wa upande wa rais Mahmoud Ahmadinejad.