TEHRAN : Ndege ya kijeshi yaanguka na kuuwa watu 36 | Habari za Ulimwengu | DW | 27.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHRAN : Ndege ya kijeshi yaanguka na kuuwa watu 36

Ndege ya kijeshi ya Iran imeanguka na kuuwa watu 36 wakiwemo walinzi 30 Kikosi cha Mapinduzi.

Televisheni ya taifa ya Iran imeripoti kwamba ndege hiyo aina ya Antonov 74 imeanguka mapema leo hii baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Mehrabad mjini Tehran katika wilaya ya magharibi ya mji mkuu huo na kuongeza kusema kwamba walinzi 30 wa kikosi cha mapinduzi na wafanyakazi sita wa ndege walikuwemo ndani wamekufa.Repoti hiyo pia imesema watu wengine wawili walijeruhiwa na kufikishwa hospitali.

Kikosi cha Ulinzi cha Mapinduzi ni cha ngazi ya juu nchini Iran ambacho inaaminika kuwa na ushawishi mkubwa sana chini ya uongozi wa Rais Mahmoud Ahmedinejad.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com