1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Mradi wa kinyuklia wa Iran utasonga mbele

25 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOY

Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran kwa mara nyingine tena ameapa kuwa Iran haitorudi nyuma kuhusu mradi wake wa nyuklia,licha ya kukabiliwa na shinikizo la nchi za magharibi.Alipokuwa akizungumza mbele ya kundi la viongozi wa kidini, Rais Ahmadinejad alilinganisha malengo ya nyuklia ya nchi yake na treni isiyokuwa na breki.Hapo awali,makamu wa waziri wa masuala ya nje wa Iran,Manouchehr Mohammadi alisema,Iran ipo tayari kukabiliana na cho chote katika mgogoro wake na nchi za magharibi,“hata vita“. Matamashi ya waziri huyo yaliripotiwa na shirika la habari la wanafunzi la Iran-ISNA.