1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Mgawo wa petroli umeanzishwa nchini Iran

27 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnx

Iran imeanzisha mpango wa mgawo wa petroli,kwa magari ya binafsi.Kituo cha televisheni ya taifa kilitoa tangazo hilo saa chache kabla ya amri hiyo kuingia kazini.Tangazo limesema,kila mwezi, mwenye gari ataruhusiwa kununua hadi lita 100 za petroli.Hatua hiyo,imezusha hasira katika mji mkuu Tehran ambako kituo kimoja cha petroli kilitiwa moto.Kwenye vituo vingine,magari yalipiga foleni kuwahi kununua petroli,kabla ya amri hiyo kuingia kazini usiku wa manane.Lengo la hatua hiyo mpya ni kupunguza athari za vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa, dhidi ya Iran,kuhusika na mradi wake wa nyuklia. Iran ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa kabisa wa mafuta duniani,lakini hata hivyo huagizia petroli kutoka nje,kwa sababu haina uwezo wa kusafisha mafuta ya kutosha.