1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Kimbunga Gonu kimeingia nchini Iran.

7 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBu1

Televisheni ya taifa ya Iran IRIB imeripoti kuwa kiasi watu watatu wameuwawa na wengine wanane wamejeruhiwa kusini mwa Iran kutokana na kimbunga Gonu.

Hakuna taarifa za mara moja kutoka kwa maafisa zinazothibitisha ripoti hiyo ya kituo cha televisheni hata hivyo.

Hapo mapema upepo wa kimbunga hicho na mvua kubwa uliikumba Oman, na kuuwa takriban watu 12 na kuleta mafuriki katika mji mkuu Muscat.

Kimbunga hicho, ambacho ni nadra kwa eneo hilo , kimelazimisha Oman kusitisha mauzo yake ya nje ya mafuta.