1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Jalili ateuliwa kuchukua nafasi ya Larijani.

21 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Dy

Kufuatia kujiuzulu kwa mkuu wa ujumbe wa Iran unaoendesha majadiliano kuhusiana na mpango wake wa kinuklia , serikali ya nchi hiyo imemteua naibu waziri wa mambo ya kigeni Saeid Jalili kuchukua nafasi yake. Msemaji wa serikali amesema kuwa kujiuzulu kwa Ali Larijani kumekubaliwa na rais Mahmoud Ahmedinejad. Hatua hiyo haitarajiwi kuathiri mazungumzo baina ya mataifa ya magharibi na Iran kuhusiana na mpango wake wa kinuklia.

Msemaji huyo amesema kuwa Jalili atakutana na mratibu wa masuala ya sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Javier Solana , kama ilivyopangwa baadaye wiki hii. Hakuna sababu zilizotolewa kwa hatua ya kujizulu kwa Larijani . Marekani na mataifa mengine ya magharibi yanaishutumu Iran kwa kutaka kutengeneza silaha za kinuklia.