1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Iran yasema itaendelea na mradi wake wa kinyuklia hata ikiwekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa.

21 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZ3

Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad amesema serikali yake itaendelea kushughulikia mradi wake wa nishati ya kinyuklia ingawa Umoja wa Mataifa unapinga.

Kwenye hotuba aliyotoa bungeni, Rais Mahmoud Ahmadinejad alisema hata kama Baraza la Usalama la Umoja huo litatangaza maazimio kumi kupinga mradi huo, Iran haitateteleka.

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa lilipitisha azimio mwezi uliopita kuiwekea Iran vikwazo kwa kukataa kusitisha shughuli ya kurutubisha madini ya yuranium yanayotumika kutengeneza bomu la kinyuklia.

Iran imekuwa ikisisitiza kwamba mradi wake huo ni wa amani.