1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN : Iran yaruhusu kamera za uchunguzi mitamboni

11 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTM

Iran imetangaza kwamba itaruhusu uwekaji wa kamera zote za uchunguzi za Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomu katika mitambo yake wa nuklea na hiyo kutimiza sharti muhimu la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Shirika la habari la taifa IRNA limeripoti kwamba kamera zote za uchunguzi zilizotakiwa ziwekwa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya nuklea IAEA zimewekwa katika mitambo ya nuklea ya Natanz katikati ya Iran ambapo mchakato tata wa kurutubisha uranium unafanyika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Iran uwekaji wa kamera hizo utawezesha shirika hilo la IAEA kuufuatilia ipasavyo mtambo huo wa nuklea wa Natanz.