1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Iran yakanusha madai ya kuchelewa kulipa malipo

20 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQe

Iran imekanusha madai kwamba imechelewa kulipa malipo baada ya kampuni ya nishati ya nyuklia ya Urusi, Rosatom, kuitaja hiyo kuwa mojawapo ya sababu ya kusitisha kazi yake ya ujenzi katika kinu cha nyuklia cha Bushehr nchini Iran.

Kusitishwa kwa ujenzi huo huenda kukachelewesha kuanza kwa kazi katika kinu hicho, iliyopangwa kuanza mwezi Septemba mwaka huu. Iran na Urusi zimesisitiza kwamba kinu hicho kitatumiwa kutengeneza nishati ya umeme pekee.

Haya yametokea kabla mkutano uliopangwa kufanyika leo kati ya mpatanishi wa Iran katika mzozo wa nyuklia, Ali Larijani, na kiongozi wa shirika la kimataifa la kuzuia usambazaji wa silaha za nyuklia, Mohamed El Baradei.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ambalo limeiwekea Iran vikwazo kwa kukataa kusitisha urutubishaji wa madini ya uranium, limeipa Iran hadi kesho ikomeshe urutubishaji wa uranium.