1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Haniyaf atakiwa na Iran kukataa kuitambua Israel.

10 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCkm

Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad amemtaka waziri mkuu wa Palestina kutoitambua Israel na kuendelea na mapambano yake dhidi ya taifa hilo la Kiyahudi.

Kiongozi huyo wa Iran ametoa matamshi hayo baada ya mazungumzo na waziri mkuu wa Palestina Ismail Haniyah wa chama cha Hamas , ambaye yuko katika ziara ya siku nne mjini Tehran.

Ziara hiyo ya Haniyah inafuatia kuvunjika kwa mazungumzo kati ya Hamas na chama cha Fatah cha rais wa Palestina Mahmoud Abbas juu ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Abbas amesema jana Jumamosi kuwa ataitisha uchaguzi na mapema ili kupata suluhisho la mzozo huo ambao unazidi kuenea.

Lakini Hamiyah amekataa mipango hiyo ya Abbas , akisema itaongeza hali ya wasi wasi.