TBILISI: Urusi yaiwekea vikwazo Georgia | Habari za Ulimwengu | DW | 03.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TBILISI: Urusi yaiwekea vikwazo Georgia

Georgia imewaachilia huru maofisa wanne wa jeshi la Urusi waliokuwa wakizuiliwa kwa kushukiwa kuwa makachero. Lakini Urusi iliyokasirishwa na hatua hiyo ya Georgia, imeiwekea vikwazo nchi hiyo ikitaka kuiadhibu, uamuzi ambao huenda uwe pigo kubwa kwa Georgia ambayo uchumi wake bado unayumbayumba.

Wapatanishi wa mataifa ya magharibi wameishawishi Urusi iwache malumbano baada ya Georgia kuwaachilia maofisa wake katika kile ilichokiita kitendo cha kirafiki. Lakini Urusi imepuuza ushauri huo na imesema kuanzia leo itakatiza usafiri wa reli, angani na baharini na huduma za posta na Georgia.

Kukamatwa kwa wanajeshi wa Urusi na maofisa wa usalama wa Georgia kumedhihirisha hali ya wasiwasi iliyopo baina ya nchi hizo mbili. Georgia inataka kujiunga na shirika la NATO na Umoja wa Ulaya, jambo linaloitia wasiwasi Urusi ambayo inaiona Georgia kama sehemu ya eneo inalolidhibiti.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com