TBILISI : Ujerumani yapendekeza kuwa mpatanishi | Habari za Ulimwengu | DW | 20.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TBILISI : Ujerumani yapendekeza kuwa mpatanishi

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir anakamilisha ziara yake ya eneo la Caucausus leo hii kwa kuitembelea Armenia.

Anatazamiwa kulenga ziara yake hiyo kwenye mvutano kati ya Armenia na Azerbeijan juu ya eneo wanalogombania la Nagorno Karabakh ambalo kwa kiasi kikubwa linakaliwa na watu wa kabila la Waarmenia.Hadhi ya mji huo inaendelea kubakia bila ufumbuzi tokea usitishaji wa mapigano hapo mwaka 1994 baada ya vita vya miaka sita kati ya majimbo hayo mawili ya zamani ya Muungano wa Urusi.

Akitembelea Georgia hapo jana Steinmeir alilenga ziara yake hiyo kwa eneo jengine linalogombania kujitenga la Abkhazia ambapo linataka kuwa na mahusiano ya karibu na Urusi.

Steinmeir amesema Ujerumani iko tayari kuwa msuluhishi katika mzozo huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com