1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TBILISI: Serikali haitotambua matokeo ya kura ya maoni

13 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtJ

Jimbo la Ossetia ya Kusini kwa mara ya pili limepiga kura ya kutaka uhuru wake kutoka Georgia.Takriban asilimia 99 ya watu wenye haki ya kupiga kura wanataka kujitenga na Georgia. NATO,Umoja wa Ulaya na Marekani zimesema hazitotambua matokeo ya kura hiyo ya maoni.Kwa upande mwingine Urussi inasema kura hiyo inapaswa kuheshimiwa.Baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 1991 hadi 1992 vilivyopoteza maisha ya mamia ya watu na kulazimisha maelfu wengine kukimbia makwao,jimbo hilo lilijaribu kujitenga na Georgia lakini haikutambuliwa kimataifa.Rais wa Georgia,Mikhail Saakashvilli anajaribu kulidhibiti tena jimbo hilo na amesema hatotambua matokeo ya kura hiyo ya maoni.