1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania: Wakimbizi kutoka Somalia warejea leo Zanzibar

6 Julai 2012

Visiwani Zanzibar, baadhi ya waliokuwa wamekimbia ghasia za kisiasa za mwaka 2001, leo (06.07.2012) wanarejea wakitokea nchini Somalia.

https://p.dw.com/p/15SKw
Kulia: Austin Makani wa shirika la UNHCR
Kulia: Austin Makani wa shirika la UNHCRPicha: DW

Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, ndilo ambalo limeratibu kurejea kwa watu hao, miaka 11 baada ya kuikimbia nchi yao.  Amina Abubakar amezungumza na msemaji wa shirika hilo nchini Tanzania, Austin Makani, ambaye kwa sasa yuko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar akisubiri kuwapokea wakimbizi hao na kuwakabidhisha kwa serikali ya huko, na kwanza alitaka kujua hali ikoje uwanjani hapo, katika masaa haya ya mwisho mwisho kabla ya kuwasili kwa ndege iliyowabeba wakimbizi hao:

(Kusikiliza mahojiano hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri: Mohammed Khelef