Tanzania: Sensa ya watu kufanyika tarehe 26 Agosti,2012
24 Agosti 2012Matangazo
Ikiwa umesalia Muda mfupi kufikia kwenye siku yenyewe ya watu kuhesabiwa, bado kumekuwa na hali ya mitazamo tofauti baina ya wananchi wa taifa hilo ambapo baadhi wanasema kuwa hawatashiriki mchakato huo. Stumai George amezungumza na Ephraim Kwesikabo, Mkurugenzi wa sensa na takwimu za jamii katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu; NBS, nchini humo na kwanza anaelezea maandalizi yalipofikia.
(Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi: Stumai George
Mhariri: Mohamed Abdulrahman