1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania: Jee Zanzibar ni nchi? Mdahala unaendelea.

29 Julai 2008

Jee Zanzibar ni dola?

https://p.dw.com/p/Em87
Ramani ya Tanzania, vikiwemo Visiwa vya ZanzibarPicha: DW


Mabishano huko Tanzania yanaendelea kuhusu suala kama Zanzibar ni nchi ama si nchi. Wanasiasa mbali mbali, wasomi na wananchi wa kawaida katika pande zote mbili za Jamhuri hiyo ya Muungano wametoa maoni yao yanayotafautiana.

Othman Miraji alimtafuta kwa njia ya simu mtu ambaye alikuwa katibu wa mwanzo wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar punde baada ya mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, Bwana Salim Rashid. Yeye pia alikuwa shahidi muhimu wakati wa kuundwa Muungano wa Tanzania baina ya marais wa Tanganyika na Zanzibar marehemu Mwalimu Julius Nyerere na Abedi Karume.

Salim Rashid anaelezea hivi kuhusu mabishano ya sasa, zaidi ya miaka 44 baada ya mapinduzi na kuundwa muungano wa Tanzania.