Tanzania: Hongo miongoni mwa Wabunge? | Matukio ya Afrika | DW | 30.07.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Tanzania: Hongo miongoni mwa Wabunge?

Tuhuma za baadhi ya wabunge nchini Tanzania kuhongwa bado lina gonga vichwa vya habari.

Hongo katika shirika la Umeme nchini Tanzania

Hongo katika shirika la Umeme nchini Tanzania

Bado sakata la tuhuma za baadhi ya wabunge kuhongwa kwa nia ya kuyatetea makampuni ya mafuta na menejimenti ya Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), linazidi kugonga vichwa vya habari nchini humo, tena katika wakati huu ambapo inadaiwa vitendo vya rushwa vinaota mizizi katika kila nyanja. Sudi Mnette amezungumza na Prof. Benson Bana, kutoka Idara ya taaluma ya Siasa na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kwanza alimuuliza tuhuma hizo za rushwa kwa wabunge amezipokeaje?

(Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini)

Mwandishi: Sudi Mnette

Mhariri

Sauti na Vidio Kuhusu Mada