Taipei.Mke wa rais wa Taiwan akabiliwa na tuhuma za ulaji rushwa. | Habari za Ulimwengu | DW | 06.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Taipei.Mke wa rais wa Taiwan akabiliwa na tuhuma za ulaji rushwa.

Rais wa Taiwan Chen Shui-bian akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa nchi hiyo Taipei amesema kuwa atajiuzulu wadhifa wake ikiwa mke wake atapatikana na hatia ya ulaji rushwa.

Siku mbili zilizopita mke wake Wu Shu-chen alielekezewa shutuma za ubadhirifu na kughushi nyaraka.

Bibi Wu anashtumiwa kwa ubadhirifu wa dola za Kitaiwan milioni 14.8 ambacho ni kiasi cha dola za kimarekani 450,00.

Muendesha mashtaka wa serikali amesema, Rais mwenyewe anahusishwa na kashfa hiyo, lakini kutokana na kinga aliyonayo Rais hawezi akashtakiwa hadi pale atakapoachilia madaraka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com