1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taarifa za siri zapoteza.

21 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQ6I

London. Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown amekabiliwa leo na maswali makali kutoka kwa wabunge baada ya taarifa za siri za benki za karibu nusu ya wakaazi wa nchi hiyo kupotea wakati zikisafirishwa. Waziri wa fedha Alistair Darling ametangaza kuwa disc mbili zenye taarifa za masurufu yote ya watoto nchini humo zilipotea baada ya kutumwa kwa njia maalum ya posta. Wabunge wa upinzani wa chama cha Conservative wamesema kuwa serikali imesababisha kiasi cha watu milioni 25 kukabiliwa na wizi wa utambulisho pamoja na kughushiwa taarifa zao katika benki.