1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria kutangaza kuacha mapigano

Admin.WagnerD25 Oktoba 2012

Serikali ya Syria leo hii inatarajiwa kutangaza uamuzi wake wa kusitisha kwa muda mapigano kama ilivyopendekezwa mpatanisha wa Umoja wa Mataifa wa mgogoro huo Lakhdar Brahimi. huku watu wataono wakiripotiwa kuuwawa.

https://p.dw.com/p/16W9W
International peace envoy for Syria Lakhdar Brahimi (2nd R) speaks at a news conference at the Arab League headquarters in Cairo October 24, 2012. Syria said on Wednesday its military command was still studying a proposal for a holiday ceasefire with rebels - contradicting international mediator Brahimi's earlier announcement that Damascus had agreed to a truce. Also pictured are former Irish president Mary Robinson (R), former Norwegian prime minister Gro Harlem Brundtland (L) and former U.S. president Jimmy Carter. REUTERS Mohamed Abd El Ghany (EGYPT - Tags: POLITICS CONFLICT)
Mpatanishi Lakhdar BrahimiPicha: Reuters

Kundi la waasi linalojita Jeshi Huru la Syria (FSA) limehakikisha kuacha mapigano katika kipindi cha siku nne za maadhimisho ya sikukuu ya Eid al-Hajj inayoanza kesho lakini kwa masharti watatekeleza hatua hiyo, ikiwa tu upande wa serikali nao utaheshimu kwa dhati makubaliano hayo.

Msemaji wa FSA, Kanali Kassim Saad Eddine, amesema watafuatilia kwa umakini endapo majeshi ya serikali yatakuwa yanatekeleza hatua hiyo. Hata hivyo, kikundi kingine cha waasi kiitwacho al-Nusra Front, kimekwisha litupilia mbali pendekezo la Brahimi la kuacha mapigano.

Taarifa za hivi punde, kwa mujibu wa Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu la Syria, zinaeleza kwamba majeshi ya serikali yameshambulia makazi ya waasi katika viunga vya jiji la Damascus na watu watano kuuwawa. Shirika hilo lenye makao yake makuu mjini London, nchini Uingereza, limesema pia kiasi ya watu 220 waliuwawa jana katika mapigano yaliyotokea katika maeno tofauti nchini Syria.

Two civilians, escorted by a rebel fighter, carry their belongings along a street strewn with debris following fighting between government troops and rebel fighters in the Salaheddin district of the northern Syrian city of Aleppo, on October 23, 2012. The UN's World Food Programme (WFP) said it had sent food aid to some 1.5 million people inside Syria in September, up from 850,000 a month earlier, as the crisis pitting President Bashar al-Assad's regime against rebel fighters deepens. AFP PHOTO/PHILIPPE DESMAZES (Photo credit should read PHILIPPE DESMAZES/AFP/Getty Images)
Mapigano mjini AleppoPicha: PHILIPPE DESMAZES/AFP/Getty Images

Uchunguzi wa vitendo vya uhalifu

Katika hatua nyingine jopo huru linalofanya uchunguzi kuhusu tuhuma za vitendo vya uhalifu wa kivita nchini Syria linahitaji mkutano wa haraka iwezekanavyo baina yake na Rais Bashar al Assad. Mkuu wa jopo hilo mwanadiplomasia Sergia Pinheiro, amesema jopo lake linaomba kukutana na kiongozi huyo bila masharti yoyote.

Chombo cha juu kabisa cha haki za binadamu cha Umoja wa Mataifa kilimtaka Pinheiro sambamba na wanachama wengine watatu katika jopo hilo akiwemo mwendesha mashitaka wa zamani wa uhalifu wa kivita anaeheshimika wa Umoja wa Mataifa, Carla Del Ponte, kuendelea na uchunguzi wao hadi Machi mwakani.

Del Ponte, ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa zamani wa serikali ya Uswisi, amesema uchanguzi wao kwa hivi sasa unatafuta washukiwa wa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita katika kipindi hiki ambacho machafuko ya umwagikaji damu yamezidi kuongezeka nchini Syria.

Duru nyingine zinasema Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Hillary Clinton amesema kuna hatari Syria inaweza kujaza ombwe la kisiasa nchini Lebanon, na hivyo amewataka wanaisiasa wa taifa hilo kuunda serikali isio na shinikizo lolote kutoka nje. Waziri huyo wa mashauri ya kigeni amesema Marekani inamuunga mkono Rais Michel Suleiman wa Lebanon katika kuunda serikali mpya baada ya mauwaji ya afisa wa juu kabisa wa usalama wa taifa hilo, katika mripuko uliyotokea katika gari Oktoba 19.

Mwandishi: Sudi Mnette/APE/DPA
Mhariri: Mohammed Khelef