1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria itashiriki katika mkutano wa Annapolis

25 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSxO

Washington:

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amewasili Marekani hii leo kwa mazungumzo ya Annapolis kuhusu amani ya mashariki ya kati.Waziri mkuu wa Israel ameafuatana na waziri wake wa mambo ya nchi za nje Tzipi Livni.Kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina Mahmoud Abbas amewasili tangu jana Washington.Akizungumza na waandishi habari bwana Mahmoud Abbas amesema anataraji mkutano wa kimataifa wa Annapolis utakidhi mahitaji ya wapalastina ya kuwa na taifa lao.Duru za karibu na wizara ya mambo ya nchi za nje ya Syria zinasema waziri mdogo wa mambo ya nchi za nje Faysal Mekdad ataiwakilisha Syria katika mazungumzo ya Annapolis.Wakati huo huo kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Papa Benedikt wa 16 amewatoa mwito wa kuombwa dua kuomba mkutano wa Annapolis ulete tija.Mkutano wa jumanne ijayo huko Annapolis karibu na Washington unaosimamiwa na rais george W. Busha umelenga kufufua utaratibu wa amani kati ya Israel na Palastina.Vatikan inatetea pawepo mataifa mawili-La Israel na la Palastina,na kusisitiza „ufumbuzi wa kudumu unabidi uzingatie kanuni za siku za mbele za mji mtukufu wa Jerusalem.“