1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria imefanyia majaribio mfumo wa silaha za kemikali

Josephat Nyiro Charo18 Septemba 2012

Jarida la Der Spiegel la Ujerumani limeripoti jana (17.09.2012) kuwa jeshi la Syria limeufanyia majaribio mfumo wa silaha za kemikali kwa kufyetua makombora katika kituo cha utafiti jangwani kaskazini magharibi mwa nchi.

https://p.dw.com/p/16Aoe
Syrian President Bashar al-Assad delivers a speech as he leaves the Elysee presidential palace, on November 13, 2009 in Paris, after a meeting with French President focused on Middle East peace process, two days after Israeli prime minister's visit in France. AFP PHOTO BERTRAND GUAY (Photo credit should read BERTRAND GUAY/AFP/Getty Images)
Portät Bashar al-AssadPicha: Getty Images

Jarida la Der Spiegel liliripoti kwamba makombora matano hadi sita yaliyotengenezwa kubeba silaha za kemikali yalivurumishwa na vifaru na ndege katika kituo kinalojulikana kama Diraiham kwenye eneo la jangwa karibu na kijiji cha Khanasir, mashariki mwa mji wa Aleppo.

Kituo cha utafiti cha Safira kilichotumiwa kinaelezwa kuwa kikubwa kabisa nchini Syria cha kufanyia majaribio silaha za kemikali na rasmi huitwa kituo cha utafiti wa kisayansi.

Kwa mujibu wa taarifa za walioshuhudia zilizonukuliwa na jarida la Der Spiegel, maafisa wa Iran wanaoaminiwa kuwa wanachama wa Jeshi la Mapinduzi walipelekwa katika eneo hilo kwa njia ya helikopta kwa majaribio hayo.

Wanasayansi kutoka Iran na Korea Kaskazini wanasemekana wanafanya kazi katika kituo hicho kikubwa kilichozungushiwa waya wa seng'eng'e. Kwa mujibu wa mashirika ya kijasusi ya mataifa ya magharibi wanasayansi hao wanatengeneza silaha za kemikali hatari ya kufisha kama vile gesi ya sumu ya sarin na sumu ya mvuke.

Source News Feed: EMEA Picture Service ,Germany Picture Service Syria's Foreign Ministry Spokesman Jihad Makdissi speaks during a news conference in Damascus July 23, 2012. Syria will only use its chemical weapons if it faces "external aggression", but will never use them against its civilians, the country's foreign ministry spokesman said on Monday. REUTERS/Stringer (SYRIA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST)
Jihad Makdissi, msemaji wa wizara ya kigeni ya SyriaPicha: Reuters

Silaha kutumika Syria ikishambuliwa

Utawala wa rais wa Syria, Bashar al Assad, umeshasema utazitumia silaha hizo iwapo nchi hiyo itashambuliwa na mataifa ya kigeni. Kufuatia shambulizi dhidi ya washirika wa karibu wa rais Assad katikati ya mwezi Julai mwaka huu, msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Syria, Jihad Makdissi, alikuwa na ujumbe mkali kwa nchi za magharibi.

"Silaha zozote za maangamizi makubwa zinazomilikiwa na Syria kamwe hazitatumiwa dhidi ya raia wakati wa mzozo huu bila kujali kitakachotokea. Silaha hizi zitatumiwa tu wakati Syria itakaposhambuliwa na mataifa ya kigeni."

Mwezi uliopita rais wa Ufaransa, Francois Hollande, alisema matumizi ya silaha za kemikali na utawala wa Syria itakuwa sababu halali ya uingiliaji kijeshi wa mataifa ya kigeni nchini humo. Marekani nayo pia inatafakari kuhusu matukio yanayoweza kujitokeza huku vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria vikiendelea na kukiwa na uwezekano wa serikali kupoteza udhibiti wa silaha zake za kemikali.

Kwa mujibu wa wachambuzi, shehena ya silaha za kemikali za Syria, ndiyo kubwa kabisa katika eneo la Mashariki ya Kati, lakini ukubwa wake haujabainika wazi.

Mkutano wa Cairo haukuleta tija

Taarifa kuhusu silaha za kemikali za Syria ilitolewa siku ambapo nchi zinazounda kundi la mawasiliano kuhusu mzozo wa Syria zilikutana mjini Cairo, Misri. Saudi Arabia haikushiriki kwenye mkutano huo uliozileta pamoja Misri, Iran na Uturuki. Hakuna sababu iliyotolewa kwa nini waziri wa mambo ya kigeni wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Saud al Faisal, hakuhudhuria kikao hicho wala kumtuma naibu wake, Mwanamfalme Abdulaziz bin Abdullah, ambaye amekuwa akimuwakilisha baada ya kufanyiwa upasuaji mwezi uliopita.

Turkish Foreign Minister Ahmet Davutoglu (L), Egyptian Foreign Minister Mohamed Kamel Amr (C) and Iranian Foreign Minister Ali Akbar Salehi attend a news conference after a meeting regarding the Syrian crisis, in Cairo September 17, 2012. Saudi Arabia stayed away from a meeting on the Syria crisis convened by regional powers on Monday, setting back a forum grouping Iran - President Bashar al-Assad's main Middle East ally - and his leading opponents in the region. The "contact group" of Egypt, Iran, Turkey and Saudi Arabia arose from an initiative by Cairo, whose new president is looking to make his mark with what he has described as a balanced Egyptian foreign policy. REUTERS/Mohamed Abd El Ghany (EGYPT - Tags: POLITICS CIVIL UNREST)
Waziri wa kigeni wa Uturuki, Ahmet Davutoglu (kushoto), Mohamed Kamel Amr wa Misri (katikati) na Ali Akbar Salehi wa IranPicha: Reuters

Waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Misri, Mohamed Kamel Amr, alisema wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari kwamba nchi hizo zimekubaliana kukutana tena kandoni mwa mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani wiki ijayo.

Mapigano yapamba moto

Vikosi vya Syria vimevishambulia vitongoji kadhaa vya mji wa Aleppo na kukabiliana na waasi mapema leo. Mapigano makali yamezuka huko Bustan al-Qasr eneo la kusini magharibi na katika kitongoji kilichiko karibu cha Izaa. Mapigano zaidi yameripotiwa pia katika kitongoji cha Sukari eneo la kusini. Kundi la kutetea haki za binaadamu la Syria limesema mapiganao ya usiku kucha yamesababisha vifo vya raia wawili katika eneo linalodhibitiwa na waasi la Sakhur kaskazini magharibi mwa nchi. Kitongoji jirani cha Hanano kimeshambuliwa kwa mabomu.

Mwandishi: Josephat Charo/AFPE

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman