SYDNEY:Mugabe ashinikizwa kujiuzulu | Habari za Ulimwengu | DW | 23.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SYDNEY:Mugabe ashinikizwa kujiuzulu

Nchi ya Australia inatoa wito kwa Afrika Kusini kumshinikiza Rais Robert Mugabe kujiuzulu kufuatia matukio ya hivi karibuni nchini Zimbabwe.Rais Mugabe alichokoza jamii ya kimataifa wiki jana kwa kuagiza wanasiasa wa Upinzani kupigwa wakiwa katika maandamano mjini Harare.Morgan Tsvangirai kiongozi wa chama cha Movement for Democratic Change MDC pamoja na wafuasi wake walipigwa vibaya sana huku muandamanaji mmoja kupigwa risasi hadi kufa.

Kulingana na Waziri Mkuu wa Australia John Howard mataifa jirani ya Zimbabwe yanapaswa kushinikiza kumalizika kwa uongozi wa Rais Mugabe uliodumu miaka 27.

Mfumko wa bei nchini humo umefikia yapata asilimia 1800 huku miaka ya raia wa Zimbabwe ya kuishi ikiwa michache sana ulimwenguni.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com