1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SYDNEY:Bush asema kuna maendeleo nchini irak

Rais George Bush wa Marekani amesema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Sydne, Australia kwamba anaona hatua zimepigwa katka nyanja za kisiasa na kijeshi nchini Irak na amefahamisha juu ya uwezekano wa kupunguzwa kikosi cha jeshi la Marekani kutoka nchini Irak.

Waziri mkuu wa Australia John Howard mshirika mkuu wa Marekani amesema ataendelea kuunga mkono sera za Marekani nchini Irak, takriban wanajeshi 1,500 wa Australia wanahudumu nchini humo.

Rais Bush yuko nchini Australia kuhudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za Pacific na Asia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com