1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto wakimbizi baadhi yao hubakwa

8 Septemba 2015

Karibu watoto 700 ambao ni wakimbizi wanawasili kila wiki nchini Sweden bila wazazi wao, wengi wakiwa wameumia katika ajali na baadhi yao wakipata majeraha ya kimwili na kisaikolojia kutokana na vipigo wanavyopata.

https://p.dw.com/p/1GSqO
watoto wakimbizi
Watoto wakimbiziPicha: Getty Images/AFP/C. Stache

Kawaida watoto hao wadogo wengi wao wakiwa wakiume, hukamilisha safari yao ndefu kutokea mashariki ya kati, Afrika na Asia wakivuka daraja la Oresund kutokea Denmark na kuomba msaada katika mji wa wa kwanza kufika nchini Swiden wa Malmo.

Wafanyakazi katika kituo cha Malmo ambao huwasaidia watoto hao wasio na waangalizi katika siku zao za kwanza nchini humo wanaelezea jinsi baadhi yao wanapo kuwa wana majeraha kichwani au mishipa iliyovunjika wakati wanapowasili.

Mara nyingi wanapata majeraha haya wakati wanapodondoka wanapojaribu kuchupia katika malori wakijaribu kutoroka lakini majeraha hayo yanaweza pia kusababishwa na wasafirishaji hao ambao huwa wamelipwa fedha na wazazi wao kwa lengo la kuwafikisha salama katika mataifa ya ulaya kasikazini.

Baadhi ya watoto kwa mfano hupata matatizo ya kusikia baada ya kupigwa masikioni wakati wa safari hizo wakitumia cheherezo na boti ambazo nyingi zake hazina viwango vya kusafiri baharini.

Wengi wao hutokea Libya

Tumeshuhudia wengi wanaowasili wakitokea nchini Libya, wakiwemo wale ambao wamenusurika kutoka katika boti zilizozama. Alisema Meneja wa kituo hicho Kristina Rosen. Mmmoja wa watoto ambaye hakuwa na msindikizaji alimuona kaka yake akizama katika bahari ya Mediterranean.

Wakimbizi wanaoingia barani ulaya
wakimbizi wanaoingia barani ulayaPicha: picture-alliance/AP Photo/S. Palacios

Watumishi katika kituo hicho wanakisia kua karibu zaidi ya nusu ya watoto hao wanahitaji uangalizi wa kisaikolojia.

Kulingana na idadi ya watu nchini humo, Sweden inapokea wakimbizi wengi zaidi wanaotafuta hifadhi ya kisiasa kuliko taifa lingine lolote barani ulaya na idadi hiyo inaongezeka kwa kasi zaidi kutokana na wengi wa wanaokimbia mapigano nchini Syria.

Taifa hilo ambalo limekuwa likipokea wakimbizi tangu miaka ya 1970 pia limekuwa likipokea karibu theruthi ya wakimbizi watoto wasio ongozana na wazazi wao wanaowasili katika mataifa hayo ya umoja wa ulaya na idadi yao ianakadiriwa kuongezeka zaidi mwaka huu na kufikia 12,000.

Duru zinaarifu kuwa wazazi wanaweza kumudu gharama za kusafirisha mtu mmoja tu ndani ya familia, nchini Sweden, mara nyingi ili kuwaepusha na kuingizwa katika makundi ya wanamgambo wapiganaji kama vile dola la kiisilam (IS) ama Al-shabaab.

Ni idadi ndogo sana ya watoto hao huungana tena na wazazi wao.

Mji wa Malmo ambao umbali wake ni wa dk 35 tu kutokea Copenhagen kwa njia ya treni ndio bandari pekee ya kuingia Sweden kwa makundi ya watoto hao.

Baadhi yao hukutwa na wageni wakishangaa shangaa mitaani ambao huwapeleka katika mamlaka husika za mji huo huku wengine huwatafuta askari polisi ama watu wa maendeleo ya jamii na wengine huachwa na wasafirishaji katika njia zinazoelekea katika ofisi za idara ya uhamiaji.

Kufikia mwezi Aug mwaka huu watoto hao wasio na wazazi ama ndugu wanaoongozana nao wapatao 9,383 wengi wao wakiume walikuwa tayari wameomba kupata hifadhi ya kisiasa nchini Sweden wengi wao wakitokea mataifa ya Afghanistan, Eritrea, Somalia na Syria na idadi hiyo ikiongezeka zaidi katika kipindi cha majira ya kiangazi. Idadi hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za idara ya uhamiaji nchini Sweden.

Mwaka jana asilimia 29 ya watoto hao wanaotafuta hifadhi katika mataifa ya umoja wa ulaya waliingia nchin i Sweden na kufanya gharama za kuwatunza kufikia dola bilioni 1.1 kwa mwaka huu.

Watoto hao hukaa katika kituo hicho cha Malmo kwa siku chache tu kabla ya kusafirishwa kwenda katika vituo vingine nchini Sweden au kuchukuliwa na familia za malezi kama ni wadogo sana.

Duru zinaarifu pia kuwa wahudumu katika kituo hicho cha Malmo huwalea watoto hao katika mazingira ya kinyumbani zaidi kuliko kitaasisi ambapo baadhi yao hukaa sebuleni wakicheza michezo katika komputa au kutumia facebook.

Mwandishi: Isaac Gamba/RTRE

Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman