1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SUVA: Kitisho cha kuzuka mapinduzi kisiwani Fiji

4 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCme

Ripoti kutoka Fiji zinasema hali ya mvutano imezidi kuwa mbaya katika kisiwa hicho baada ya vikosi kujinyakulia silaha kutoka makao makuu ya kituo cha polisi.Mkuu wa majeshi,Voreqe Bainimarama,alipozungumza na waandishi wa habari alisema,jeshi limewapokonya silaha walinzi wa waziri mkuu Laisenia Qarase na wa mawaziri wake. Inahofiwa kuwa kuna hatari ya kufanywa mapinduzi baada ya vikosi kuziba barabara katika mji mkuu Suva.Lakini Bainimarama amekataa kusema ikiwa mapinduzi yapo njiani.