1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Suu Kyi: ''Sina chuki na utawala wa kijeshi''.

Halima Nyanza14 Novemba 2010

Kiongozi wa upinzani nchini Myanmar ambaye ameachiliwa huru jana baada ya kuwa kizuizini kwa miaka kadhaa Aung San Suu Kyi, amesema hana chuki na utawala wa kijeshi nchini humo, ambao ndio ulikuwa ukimshikilia.

https://p.dw.com/p/Q8FQ
Kiongozi wa upinzani Myanmar, Aung San Suu Kyi.Picha: AP

Katika hotuba yake ya kwanza baada ya zaidi ya miaka saba, aliwaambia maelfu ya wafuasi wake leo, kwamba anataka kufanya kazi pamoja na vyombo vyote vya kidemokrasia, ili kuweza kuboresha maisha ya watu Myanmar, ambayo ni moja ya nchi masikini kabisa kusini mashariki mwa Asia.

Aung San Suu Kyi
Wafuasi wake wakishangilia kuachiwa kwake.Picha: picture-alliance/dpa

Jana Jumamosi viongozi wa nchi mbalimbali duniani walipongeza kuachiliwa huru kwa Suu Kyi, baada ya zaidi ya miaka 15 ya kifungo cha  gerezani na nyumbani.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, amesema msimamo wa Suu Kyi wa kutopenda ghasia na wa kutokukata tamaa umemfanya apendwe na watu.

Angela Merkel Belgien Brüssel Yves Leterme
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ni miongoni mwa viongozi wa kimataifa, waliopongeza kuachiliwa huru kwake.Picha: AP

Nye Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Ujerumani Guido Westerwelle ameutaka uongozi wa kijeshi nchini Myanmar kuchukua hatua zaidi.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban KI Moon, amemuelezea Suu Kyi kama kichocheo cha matumaini duniani.