Suharto kiongozi wa zamani Indonesia yuko mahtuti | Habari za Ulimwengu | DW | 14.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Suharto kiongozi wa zamani Indonesia yuko mahtuti

JAKARTA

Ndugu wa familia wamesema watawaachilia madaktari waamuwe iwapo Rais wa zamani wa nchi hiyo Suharto aondolewe mashine za kumsaidia uhai baada ya viungo vyake vyote kushindwa kufanya kazi.

Madaktari wameelezea hali yake kuwa mbaya sana. Suharto mwenye umri wa miaka 86 amekuwa na matatizo makubwa ya moyo mapafu na mafigo na amekuwa akisadiwa kupumuwa na mashine.

Madaktari wamesema uwezekano wa kiongozi huyo wa zamani wa Indonesia ambaye amekimbizwa hospitali hapo tarehe nne Januari kuendelea kuishi ni asilimia hamsini kwa hamsini.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com