STUTTGART: Magaidi wasiwe na uhuru wa kutenda watakavyo | Habari za Ulimwengu | DW | 22.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

STUTTGART: Magaidi wasiwe na uhuru wa kutenda watakavyo

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anaunga mkono pendekezo la kuruhusu upelelezi wa mawasiliano ya kompyuta za binafsi katika kupiga vita ugaidi. Alipozungumza kwenye mkutano wa chama chake cha CDU mjini Stuttgart Merkel alisema,magaidi wasiachiliwe uhuru wa kutenda watakavyo,bila ya dola lenye utawala wa kisheria,kuweza kuchukua hatua.

Ujerumani katika miaka ya hivi karibuni, imenusurika na mashambulizi saba yaliyopangwa kufanywa nchini humu.Kansela Merkel amesema,hicho ni kitisho cha aina mpya.Haiwezekani tena kutenganisha usalama wa nje na wa ndani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com